Watanzania waipaisha nchi kimataifa, wafanya mambo mazuri wikiendi hii.

Watanzania waipaisha nchi kimataifa, wafanya mambo mazuri wikiendi hii.

01 Oct, 08:32

Ni wikiend nyingine ya Nyota wa Tanzania wakiendelea kuitangaza vyema nchi katika mataifa mbalimbali ambayo wanacheza soka la kulipwa.


Mbwana Samatta ambaye ni balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji katika Klabu ya KRC Genk jana ameshindwa kuisaida timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya Eupen FC baada ya kulazimisha sare ya mabao 3-3 na kuendelea kujiweka pabaya katika msimamo wa ligi ya nchini hiyo.

Samatta akicheza kwa dakika zote 90 ameshuhudia Timu yake ikitoka nyuma na kusawazisha mabao yote matatu kupitia kwa Marcus Ingvarten dakika ya 53, Siebe Schrijevers katika dakika ya 66 na Marcus Ingvarten tena katika dakika ya 78.

Mabao ya wenyeji katika mchezo huo yalifungwa na Siebe Blondelle, Akram Afif na Mbaye Leye na kuwafanya Genk ya Mbwana Samatta kufikisha alama 10 katika michezo 9 wakikalia nafasi ya 9 kwenye ligi yenye jumla ya timu 16.

Michael Lema.

Kwenye Bundesliga ya Austria Mtazania mwingine Kinda Michael Lema ameendelea kukaa nje ya uwanja kutokana na majeraha aliyoyapata mwezi Agosti hivyo kushindwa kuchangia timu yake ya Strum Graz katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya SKN St. Poelten.

Lema ambaye alipandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Strum Graz akitoke kwenye academy ameshindwa kabisa kucheza mchezo wowote hadi hivi sasa labda ni kutokana na majeraha pamoja na ushindani wa namba.

Hata hivyo Timu yake ndiyo inayoongoza ligi kwa sasa wakiwa na alama 22 baada ya michezo 10, kwa kufikisha alama 22 ambazo ni sawa na kushinda michezo saba, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Farid Musa.

Mtanzania mwingine Farid Musa atakuwa mzigoni leo jioni kuitumikia timu yake ya CD Tenerife inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uhispania pale watakapokwaana na Lugo kuanzia majira ya saa moja jioni katika uwanja wa Estadio Anxo Carro.

Tenerife inashuka katika mchezo huo wakiwa wamekwishacheza michezo 6, ambapo kati ya hiyo wamepoteza michezo miwili wakishinda michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja matokeo yanayowapa pointi 10 na kukalia nafasi ya 7.

Abdi Banda.
Nchini Afrika Kusini, mlinzi wa kati wa Tanzania Abdi Banda jana ameisaidia Timu yake ya Baroka FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu kongwe na tajiri nchini humo ya Kaizer Chiefs.

Banda amecheza dakika zote 90 katika mchezo huo ambao ulifanyika kwenye uwanja wa Moses Mabhida, uliopo Durban na kushuhudia mabao ya Timu yake yakifungwa na Lewis Macha katika dakika ya 23 pamoja na Gift Motupa katika dakika ya 59, wakati lile la kufutia machozi la Kaizer Chiefs likifungwa na George Maluleka katika dakika ya 9.

Matokeo hayo yanawafanya Baroka FC kufikisha alama 15 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo huku pia wakiendeleza rekodi nzuri ya kutoruhusu kupoteza katika michezo 7 ambayo wameshuka dimbani hadi hivi sasa.

Simon Msuva.

Na kule nchini Morocco pambano kati ya Difaa El Jadida ya Simon Msuva na Wydad Casablanca umesogezwa mbele kutokana na ushiriki wa Casablanca katika michuano ya Klabu bingwa barani Afrika.

Pambano hilo lilipangwa kufanyika Leo na lingekuwa ni pambano la tatu kwa Msuva kuichezea timu yake ya Difaa El Jadida inayoshika nafasi ya 7 katika ligi yenye timu 16, ikiwa na alama 4 baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja.

Related news
related/article
International News
UEFA CL: Real Madrid v Liverpool in numbers
25 May, 14:50
International News
Fred to keep United waiting
25 May, 08:55
International News
Ex-Manchester United star advises Martial
23 May, 17:55
International News
Koscielny reveals his remedy to World Cup heartache
24 May, 16:40
International News
Fairytale ending could be in the script, says World Cup-bound Vardy
24 May, 14:24