Mkutano wa Klabu ya Simba waja na Maamuzi mazito.

Mkutano wa Klabu ya Simba waja na Maamuzi mazito.

13 Aug 2017, 15:59

Wanachama wa Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam wamekutana Leo katika mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere international Conference Centre).

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kufanya mikutano yake katika Ukumbi wa hadhi hiyo uliopo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM) Maamuzi kadhaa yamefikiwa.

Moja ya Maamuzi hayo ni pamoja na kuwasamehe Wanachama 71 waliowahi kupeleka Shauri mahakamani Lakini Kwa sharti La kufuta kesi hiyo.

Pia Kamati ya utendaji ya Simba imemuondoa Mzee Kilomoni kwenye baraza la wadhamini kwa kupeleka kesi katika mahakama za kawaida.

Pamoja na kuondolewa kwenye udhamini, Mzee Hamis Kilomoni amesimamishwa uanachama na asipofuta kesi Mahamakani na kuomba radhi atafutwa kabisa.

Aidha Simba pia Kwa kauli moja imemteua Adam Mgoyi (Mkuu wa Wilaya ya Kilosa) kuwa mdhamini mpya wa klabu kuchukua nafasi ya Mzee Kilomoni kwenye baraza la wadhamini.

Mkutano huo pia umemthibitisha Juma Othuman Kapuya kuwa mdhamini wa klabu kuziba pengo la mzee Ally Sykes aliyefariki dunia Mwaka 2013.

Pongezi kwa Wallace Karia. 

Katika mkutano huo ulioongozwa na Kaimu Rais wa klabu hiyo Salim Abdallah 'Try Again' limempongeza Wallace Karia kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini 'TFF' na kuahidi ushirikiano.

Nyange Kaburu na Evance Aveva. 

Pia wamewatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa bado wanawatambua Viongozi wao Rais Evance Aveva na Makamu Geofrey Nyange Kaburu Licha ya kuwa mikononi mwa Dola.

-Bado tunawatambua viongozi wetu wakuu Rais Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange kwakua bado hawajukutwa na hatia," amesema Kaimu Rais Salim Abdallah.

Kuhusu kuelekea katika Mfumo wa kampuni Salim Abdallah amesema "Simba ikifanikiwa kuingia kwenye mfumo wa uendeshwaji kwa hisa itakuwa klabu namba mbili Afrika kwa thamani,".

Kombe la Shirikisho Afrika. 

Mwisho Viongozi wa klabu hiyo wamesema lengo lao msimu ujao Ni kushiriki vyema michuano ya Afrika ikiwemo kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

-Simba imejipanga kuhakikisha inatwaa kombe la Shirikisho Afrika ndio maana imesajili kikosi bora zaidi Afrika Mashariki," amesema Salim Abdallah.

Mkutano huo umehudhuriwa na Wanachama zaidi ya 950 na Mara baada ya mkutano Wote wameelekea uwanja wa Taifa kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Kirafiki.

Related news
related/article
FIFA World Cup
Pitch invaders jailed for World Cup final act
12 hours ago
FIFA World Cup
Fifa investigates ‘possible discriminatory’ England fan chants
13 Jul 2018, 08:50
Transfer News
Rumour: Mbappe on Manchester United's radar?
14 hours ago
English Premier League
New Chelsea coach to make a few adjustments
16 Jul 2018, 18:40
Transfer News
Martinez hints at Hazard future
16 Jul 2018, 21:35