Makamu wa Rais wa TFF matatani kwa matumizi mabaya ya ofisi

Makamu wa Rais wa TFF matatani kwa matumizi mabaya ya ofisi

14 Mar 2018, 15:04

Kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imekutana Jumatano Machi 14, 2018 pamoja na mambo mengine kamati hiyo itajadili suala la Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Michael Richard Wambura aliyefikishwa kwa masuala ya kimaadili.

Shauri hilo la Wambura limefikishwa kwenye kamati ya Maadili na Sekretarieti ya TFF baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo mbalimbali ya ukaguzi na suala hilo la Wambura kuonekana linatakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili.

Kamati ya Maadili imepokea malalamiko yanayomuhusu Wambura ikiwa ni uvunjifu wa kanuni za Maadili Tolea la 2013 na Katiba ya Shirikisho hilo kama ilivyorekebishwa mwaka 2015.

Wito huo umemtaka Wambura kufika mbele ya Kamati ya Maadili ili kutoa utetezi huo kwa njia ya mdomo, ama kutuma kwa maandishi, au kuleta mashahidi au kutuma muwakilishi akiambatana na barua ya uwakilishi.

Makosa anayoshtakiwa Wambura ni

1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanui za Maadili za TFF Toleo la 2013

2.Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013

3.Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)

Related news
related/article
FIFA World Cup
Nigeria fall short as Croatia grab top spot
16 Jun 2018, 21:57
International News
Wilshere drops huge hint about Arsenal future
14 Jun 2018, 09:25
FIFA World Cup
Ugandan-born-Dane makes World Cup debut against Peru
16 Jun 2018, 17:15
International News
A growing trend? Poor starts for World Cup champions
8 hours ago
FIFA World Cup
How South Korea plan to confuse Sweden
11 hours ago