Mtibwa Sugar yawatuliza mashabiki yaahidi kufanya makubwa

Mtibwa Sugar yawatuliza mashabiki yaahidi kufanya makubwa

14 Mar 2018, 09:00

Klabu ya Mtibwa Sugar ya kutoka mkoani Morogoro imekiri kusikitishwa na matokeo mabaya Timu hiyo imekuwa ikionyesha na kuwaomba mashabiki wa timu hiyo kuwa wavumilivu wakati wakiendelea  kujipanga upya ili kuimarisha timu hiyo. 

Akizungumza na futaa.co.tz Msemaji wa Klabu ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema wanaelewa masaibu wanaopitia mashabiki wao kufuatia matokeo hayo na kuwaahidi matokeo mazuri katika michezo ijayo ga ligi kuu na pia FA.

 "Hatujafanya vyema toka kuanza kwa msimu wa pili wa ligi kuu tumepoteza michezo minne ni bahati mbaya ni upepo mbaya, tunajipanga upya imetusikitisha naamini sio sisi tu lakini mashabiki na wadau wetu pia ndani na nje ya Tanzania ni upepo tu ambao umevuma kwetu naamini utatulia", amesema Kifaru.

 Kifaru amesema wameweka yote nyuma na kwa sasa nguvu yote wanaiwekeza kwenye michezo ijayo.

"Tumerejea Morogoro ambapo tunaendelea na mazoezi tunakabiliwa na michezo mitatu migumu dhidi ya Azam Fc mchezo wa FA na miwili ya ligi ambapo watakabiliana na Yanga na Simba SC, niwaombe mashabiki wetu wawe na subira wakati tukijipanga upya kufanya mikakati mikali ili kuwafuta machozi mashabiki wetu kuhakikisha tunashinda michezo hio yote", ameongeza Kifaru. 

Mtibwa Sugar ambao wanashika nafasi ya 6 wakiwa na alama 27 hawajapata ushindi katika michezo hao mitano ya mzunguko wa pili wakipoteza dhidi ya Stand United, Mwadui Fc, Ruvu Shooting na Tanzania Prisons wakitoka sare na Mbao Fc. 

Related news
related/article
FIFA World Cup
WC 2018: Mexico to trouble Germany
14 Jun 2018, 08:00
International News
Liverpool target pours cold water on exit reports
12 Jun 2018, 14:30
FIFA World Cup
Mini-earthquake reported in Mexico due to celebrations
10 hours ago
FIFA World Cup
Ronaldo matches Pele, Puskas' records
16 Jun 2018, 07:05
FIFA World Cup
Messi misses penalty as Iceland holds dominant Argentina
16 Jun 2018, 15:54