Simba mambo ni hivi, mambo ni moto

Simba mambo ni hivi, mambo ni moto

04 Feb, 17:48

Wekundu wa msimbazi Simba SC imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya soka ya Ruvu Shooting katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba wakionekana wanauchu wa kupata ushindi katika mchezo huo, walipata bao lao la kwanza kupitia kwa John Bocco katika dakika ya 21 baada ya kuonganisha kwa kichwa mpira wa kona uliochongwa na Shizya Kichuya.

Simba waliandika bao la kupitia kwa Mzamiru Yassin katika dakika ya 66 kufuatia krosi sukari ya Shizya Kichuya na kama hiyo haitoshi Simba waliandika bao la tatu katika dakika ya 75 ya mchezo huo kupitia kwa John Bocco Adebayor. 

Mbao 2-1 Kagera

Jijini Mwanza wabishi Mbao FC wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa jasho na damu wa mabao 2-1 dhidi ya wanankurukumbi Kagera Sugar katika mchezo ambao umefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko mambo yalikuwa ni nyau nyau lakini hali ilibadilika katika kipindi cha pili ambapo Mbao walipata bao la kwanza kupitia kwa James Msuva kwa guu la kushoto nje ya 18 lililomshinda kipa Juma Kaseja.

Katika dakika ya mshambuliaji hatari Habibu Kiyombo alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Emmanuel Mvuyekule huku Kagera Sugar wakipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 74 kupitia faulo ya moja kwa moja ya Atupele Green.

Stand 2-1 Mtibwa

Mjini Shinyanga, Stand United wameendelea kuwa wamoto mara hii wakiwafunga Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 mchezo ambao umepigwa katika nyasi za uwanja wa CCM Kambarage.

Mtibwa ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 25 kupitia kwa Salumu Kihimbwa lakini Stand wakasawazisha kupitia kwa Bigirimana Babibakule na baadae kuongeza la pili katika dakika ya 87 kupitia kwa Tariq Seif.

Msimamo.

Mpaka raundi ya 16 inahitimishwa Simba wanaendelea kuwa kileleni wakiwa na alama 38, Azam wakifuatia kwa kukusanya alama 33 wakati Yanga wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 31.

Mkiani wapo Kagera Sugar waliopo katika nafasi ya 14 wakiwa na alama 13 sawa na Njombe Mji waliopo katika nafasi ya 16 na Majimaji waliopo katika nafasi ya 15.

Related news
related/article
International News
Klopp proud of Liverpool
22 hours ago
International News
WC 2018: Liverpool youngster not overwhelmed by England call-up
22 hours ago
International News
Herrera: United continuing to improve under Mourinho
19 May, 08:40
International News
Ranieri open to offers
20 May, 15:55
International News
Celtic complete historic double treble by seeing off Motherwell
19 May, 17:10