Msuva ashindwa kuisaidia timu yake, yachezea kichapo

Msuva ashindwa kuisaidia timu yake, yachezea kichapo

24 Dec, 14:20

Timu ya Difaa El Jadida inayoshiriki ligi kuu ya nchini Morocco ‘Batola Pro’ anayochezea mshambuliaji Mtanzania Simon Msuva imedondoshwa hadi nafasi ya nne kwenye msimamo baada ya hapo jana kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Ittihad Tanger.

Bao pekee la Tanger katika mchezo huo limefungwa na Khalid Serroukh kwa njia ya penati katika dakika ya 38 ya mchezo huo ambao umefanyika kwenye uwanja wa Manispaa mjini Tangier.

Huu unakuwa mchezo wa pili kwa El Jadida kupoteza msimu huu, kwani ikumbukwe Novemba 29 walipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa FUS Rabat.

Msimamo ulivyo.

Difaa El Jadida sasa inakamata nafasi ya nne baada ya kukusanya alama 20 ambapo iliyowafunga  yenyewe inapanda hadi nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 21 katika  michezo 13 ambayo kila timu tayari imecheza.

Katika msimamo wa ligi hiyo ambayo inashirikisha jumla ya timu 16 Hassania Agadir ‘HUSA’ inaongoza ikiwa na alama 23 baada ya kucheza michezo 12 huku Raja Casablanca wakiwa nafasi ya tatu kwa alama 21 baada ya michezo 11.

Related news
related/article
International News
Iniesta: I arrived as a boy, I leave as a man
21 hours ago
International News
Bordas: Neymar regrets PSG move
18 May, 15:30
International News
Asamoah announces Juventus exit
18 May, 06:25
International News
Ranieri open to offers
20 May, 15:55
International News
Fan shows off Monk face tattoo on bottom
20 May, 15:49