2018 Women WCQ: The Tanzanite kurejea mapema kujiandaa na Nigeria.

2018 Women WCQ: The Tanzanite kurejea mapema kujiandaa na Nigeria.

18 Sep, 13:18

Kikosi cha timu ya Taifa ya Soka ya wanawake kwani waliochini ya umri wa miaka 20 'The Tanzanite' kinatarajiwa kurejea nchini usiku wa kuamkia jumanne kikitokea Nigeria.

Mara baada ya kuwasili nchini kikosi hicho kitaelekea moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia dhidi ya Vijana wa Nigeria 'Falconets', Septemba 29 Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza Tanzania walipoteza kwa mabao 3-0 mchezo ambao ulifanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Samuel Ogbemedia Mjini Benin katika Jimbo la Edo, nchini Nigeria.

Kipigo cha 3-0.

Mabao ya wenyeji katika mchezo huo yalifungwa na Rasheedat Ajibade Aliyefunga mabao mawili katika dakika ya 52 na 57 na Lilian Tule aliyefunga dakika ya 22.

Kwa mantiki hiyo Tanzania watahitaji ushindi wa zaidi ya mabao manne ili Kufuzu na kucheza na mshindi kati Morocco au Senegal katika hatua inayofuata.

The Tanzanite wanatafuta nafasi ya kufuzu kwenye fainali za Kombe la dunia kwa mara ya kwanza, fainali ambazo zitafanyika mwakani nchini Ufaransa.

Related news
related/article
International News
Gerrard: Liverpool players can change their lives
6 hours ago
International News
FIFPro appeals to FIFA overWorld Cup ban
21 hours ago
International News
Willian takes dig at Conte?
20 May, 15:50
International News
Mijatovic advises Real Madrid against Salah move
19 May, 16:01
International News
Valverde sees no way of replacing Iniesta
19 May, 17:20