Uchaguzi TFF: Wallace Karia aibuka kidedea, kurithi mikoba Ya Jamal Malinzi.

Uchaguzi TFF: Wallace Karia aibuka kidedea, kurithi mikoba Ya Jamal Malinzi.

12 Aug 2017, 18:02

Mgombea nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka nchini Wallace Karia amefanikiwa kunyakuwa kiti hicho baada ya Kuwashinda wagombea wengine watano katika Uchaguzi mkuu uliofanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa St Gasper Mjini Dodoma.

Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Wakili Revocatus Kuuli, amemtanga Wallace Kalia kuwa mshindi baada ya kuwashinda Wenzake kwa kupata kura 95 kati ya kura halali 125 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF ambazo ni sawa na aslimia 76 ya kura zote zilizopigwa.

Aliyetazamiwa kuwa mpinzani wa karibu wa Karia katika Uchaguzi huo mchezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa na klabu ya Yanga Ally Mayay amepata kura 9 ambazo ni sawa na asilimia 7.2 za kura zote.

Aidha Richard Shija naye amepata kura 9 katika uchaguzi huo ambazo ni sawa na asilimia 7.2, huku Iman Madega ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Yanga akipata Kura 8 ambazo ni sawa na asilimia 6.4 za kura zote.

Katibu mkuu mkuu wa zamani wa TFF, Fredrick Mwakalebela amepata kura 3 ambazo ni sawa na asilimia 2.4 huku katibu mkuu wa Klabu ya Mbeya City Emmanuel Kimbe akipata kura 1 ambayo ni sawa na 0.8 ya kura zote.

Makamu wa Rais.

Katika nafasi ya Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa wa Mara Michael Richard wambura ameibuka Kidedea baada ya 85 katika uchaguzi huo na kuwamwaga Mulamu Nghambi, Mtemi Ramadhan Stephen Mwakibona na Robert Selasela waliokuwa wakiwania pamoja naye.

Kamati ya Utendaji.

Kwa upande wa kanda 13 za TFF walioshinda ni Saloum Chama kwa Kanda namba 1 (Geita na Kagera), Vedastus Lufano kanda namba 2 (Mwanza na Mara), Mbasha Matutu amechukua kanda namba 3 (Shinyanga na Simiyu), Sarah Chao naye amechukua kanda namba 4 (Arusha na Manyara).

Wengine ni Issa Bukuku aliyeshinda kanda namba 5 (Tabora na Kigoma), Kenneth Pesambili amechukua kanda namba 6 (Katavi na Rukwa), Elias Mwanjali ameibuka kidedea kwa kanda namba 7, James Mhagama yeye amechukua uongozi wa kanda namba 8 (Njombe na Ruvuma) na Dustan Mkundi amechukua kanda ya 9 (Lindi na Mtwara).

Mohamed Aden ameibuka mshindi kwa kanda namba 10 (Dodoma na Singida), huku Francis Ndulane akichukua uongozi wa kanda namba 11 (Pwani na Morogoro), Khalid Abdallah yeye amechukua ushindi wa kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) na Lameck Nyambaya ameibuka kidedea kwa kuchukua kanda ya 13 inayowakilisha Mkoa wa Dar es Salaam.

Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ya Uchaguzi Viongozi wote wameapishwa mbele ya Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa ‘BMT’ Mohamed Kiganja na Msajili wa vyama vya michezo kama agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe.

Related news
related/article
English Premier League
Arsenal boss ready to get best out of Ozil
14 Jul 2018, 07:25
English Premier League
Pre-season: Liverpool goalkeeper makes another mistake
11 Jul 2018, 06:00
FIFA World Cup
Casillas, Suarez criticize VAR use in World Cup final
1 hour ago
FIFA World Cup
Hazard speculates his future
15 Jul 2018, 16:45
English Premier League
Silva hopes Everton will deliver on transfer targets
8 hours ago